HabariUncategorized

Mke na Mume wafariki kwa kunywa chai ya rangi

Familia moja, mke na mume waliokuwa wakiishai katika wakazi kijiji cha Baga. Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, wamefariki dunia baada ya kunywa chai ya rangi inayodhaniwa kuwa na sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, alithibitisha kutokea tukio hilo siku ya Juni 19, mwaka huu saa saba mchana wakati familia hiyo ilipoandaa kinywaji hicho.

Kamanda Wakulyamba amesema katika tukio hilo, Ndugu Rajabu Ally (73) na Amina Rajabu (62) walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika Zahanati baada ya kunywa kinywaji hicho, hata hivyo mpwa wao Adam Saidi (12), mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Mashine, alinusurika kifo.

“Tukio hilo limepoteza watu wa familia moja, mpwa wao alinusurika baada ya kunywa chai idhaniwayo kuwa ni yenye sumu, tunaendelea na upelelezi wa tukio hili,” alisema Kamanda Wakulyamba.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents