Habari

Mke wa rais wa zamani wa Marekani George HW Bush, Barbara afariki dunia

Mke wa zamani wa rais wa Marekani, George HW Bush, Barbara Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.


Barbara Bush akiwa na mumewe George H.W. Bush March, 2017

Barbara ambaye pia ni mama mzazi wa George W Bush, amekuwa akidorora kiafya kwa muda sasa na alikuwa amekataa kupatiwa matibabu zaidi.

Katika taarifa ambayo ilitolewa na George W Bush, amesema, “Mama yangu mpendwa ametuwacha akiwa na umri wa miaka 92. Laura Barbara, Jenna na mimi tunaomboleza , lakini roho zetu zimepumzika kwa sababu tunajua yake pia imepumzika.

Inatajwa kuwa Barbara ndiye aliyekuwa nguzo muhimu ya kisiasa katika uongozi wa mumewe George HW Bush na mwanawe George W Bush.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents