Mke wa Tarzan achomwa kisu, mtoto wake apigwa risasi na kufariki papo hapo

Mtoto wa kiume wa nyota wa filamu ya Tarzan iliyojizoelea umaarufu mkubwa miaka 60, Ron Ely ameripotiwa kumchoma kisu mama yake mzazi na kumsababishia kifo wakiwa nyumbani kwao, California siku ya Jumanne jioni.

Ron Ely and his wife Valerie Lundeen at a tennis match in New York City in June 1977

Polisi walifika nyumbani kwa sta huyo ambayo ipo kwenye mtaa wa Santa Barbara na kuupata mwili wa marehemu, Valerie Lundeen Ely mwenye umri wa miaka 62 ukiwa na majeraha ya kuchomwa na kisu.

Hata hivyo polisi waliweza kumpiga risasi mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 30 na kufariki baada ya kuhofia usalama wa raia wengine.

Hakuna taarifa yoyote juu ya muigizaji huyo wa filamu ya Tarzan mwenye umri wa miaka 81 kuwa amejeruhiwa ama laa.

Ron Ely plays Tarzan in the television series of that name, circa 1967Ron Ely ameigiza Tarzan katika kipindi cha televisheni mnamo 1967

Lakini hapo awali ofisi ya mkuu wa polisi ilieleza kuwa mwanamume mtu mzima mlemavu aliyekuwepo ndani ya nyumba hiyo amepelekwa hospitalini kufanyiwa ukaguzi.

Taarifa ya hivi punde ya idara hiyo ya polisi Santa Barbara imesema: “Maafisa waliipekuwa nyumba na maeneo ya karibu kumtafuta Cameron Ely.

“Wakati wa upekuzi huo, mtuhumiwa alipatikana nje ya nyumba. “Alikuwa tishio maafisa wannne walimfyetulia silaha mshukiwa na kumuua.”Ron Ely poses for the 1966 Tarzan TV series

Ron Ely mnamo 1966 katika makala ya Tarzan

Ron Ely anafahamika pakubwa kwa kuigiza kipindi cha Tarazan kilichopeperushwa kati ya 1966-68. Tarzan alikuwa ni mshiriki katika kipindi hicho aliyelelewa na nyani katika jangwa la Afrika, katika kitabu cha Edgar Rice Burroughs kilichochapishwa mnamo 1914.

Ely apia aliigiza kama muigizaji mkuu katika filamu ya mnamo 1975 Doc Savage: The Man of Bronze. Bi Lundeen alikuwa mlimbwende aliyeshinda taji la Miss Florida.

Wawili hao wana mabinti wawili pia, Kirsten and Kaitland. Ron Ely alipumzika uigizaji kati ya 2001-14 kabla ya kurudi na kushiriki katika filamu ‘Expecting Amish’.Actor Ron Ely in 2012

Ron Ely mnamo 2012

Ameliambia jarida la Charlotte Observer wakati filamu hiyo ilipotoka kwamba: “NIlisitisha uigizaji kuilea familia yangu na kuoata fursa ya kukaa nao zaidi hapa Santa Barbara.

Muigizaji huyo pia aliandika vitabu viwili, Night Shadows, mnamo 1994, na East Beach, alichokiandika mwaka mmoja baadaye.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW