Burudani

Mke wangu ni mganga wa jiko – Dogo Janja

Msanii wa muziki Bongo, Dogo Janja amefunguka kinachomvutia kutoka kwa mke wake Irene Uwoya msimu huu wa wapendanao (valentine).

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Ngarenaro’ ameiambia ITV kwa sasa anavutika zaidi na mapishi ya mkewe.

“Vyakula anavyonikipia mke wangu hatari sana, fundi jikoni, mganga wa jiko. Ni mwanamke mwenye vision, ni mtu ambaye tunaelewana, tunasikilizana, ni marafiki,” amesema Dogo Janja.

Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa November mwaka jana, 2017 hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili ya ndoa hiyo kutokana na namna walivyoliweka suala hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents