Burudani

Mkenya atwaa ushindi Tusker Project Fame 5


Ruth Matete wa Kenya jana ameibuka mshindi kwenye shindano la Tusker Project Fame Season 5.
Muimbaji huyo amepata kitita cha shilingi milioni 5 za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 90 za Kitanzania.
Katika fainali hizo za jana usiku, mshindi wa pili amekuwa Doreen wa Uganda, Jackson wa Rwanda akikamata nafasi ya tatu na Joe wa Burundi akishika mkia kwa kuibuka wanne.
Pamoja na kitita hicho Ruth amepata deal ya kufanya kazi na label kubwa duniani ya Universal Music Group.
Hata hivyo kuna watu wana mashaka kuwa muonekano wa Ruth ambao si wa ki ‘Hollywood’ unaweza usimpe mafanikio kimuziki.
Alipotajwa kuwa ndiye mshindi wa mwaka huu alishindwa kuongea chochote na hivyo kuanguka chini na kuanza kumshukuru Mungu. Walioshindwa walikubali matokeo na kuahidi kuendelea kufanya muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents