Michezo

Mkenya aweka rekodi mbio za Diamond League

Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 18, Celliphine Chespol amefanikiwa kushinda mbio za mita 3000 kuruka maji na viunzi katika mashindano ya Prefontaine Classic Diamond League.

Mkenya huyo alitumia muda wa dakika 18 sekunde 58.57 licha ya kuwa hakuvaa vizuri kiatu chake cha mguu wa kulia katika raundi ya mwisho,Kutokana na ya kupoteza kiatu chake kwa muda.

Mshindi wa pili katika mbio hizo alikuwa ni Beatrice Chepkoech,huku Ruth Jebet kishikiria nafasi ya tatu katika mio hizo

Mbio zingine zamita 5, 000 mwanariadha wa Ethiopia Genzebe Dibaba alishindwa kuvunja rekodi ya dadake Tirunesh Dibaba.Bingwa huyo mwenye umri wa miaka 26 alishinda mjini Eugene Oregon kwa dakika 14 na sekunde 25.22 ikiwa ni sekunde 14 nyuma ya muda uliowekwa na dada yake 2008.

“Nina furha nimeshinda ila sina sijafurahishwa na muda”amesama Dibaba mwanariadha tokea EthiopiaNae mkenya aliepoteza kiatu alisema “Sijafurahi jinsi nilivyoanza mashindano. Nilihisi kupoteza leo katika mbio hizi na haikuwa rahis kushinda”ameeleza Chespol mshindi tokea Nchini Kenya aliepoteza kiatu chake katiaka raundi ya musho ila hakukubali kukata tamaa hatimaye akaibuka mshindi wa mbio hizo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents