Habari

Mkinichagua mtatibiwa bure – Mgombea Urais NRA, Ndg Leopard Lucas Mahona

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoka chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Leopard Lucas Mahona, ameahidi kuwa endapo akipewa ridhaa na watanzania kuwatumikia katika Uchaguzi wa Oktoba 28, 2020, atahakikisha huduma za afya zinatolewa bure.

Mgombea Urais kupitia chama cha NRA Leopard Mahona.

Mahona amesema hayo hii leo Septemba 3, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akinadi sera zake katika Soko la Kariakoo, na kuongeza kuwa huduma bure za afya zitatolewa kwa watu wote bila kuzingatia umri, kama ambavyo hali ilivyo kwa sasa kwani wanaotibiwa bure ni wazee pekee.

“Nitahakikisha hakuna gharama yoyote mnayolipa, hata senti moja hamtatozwa, Watanzania mtapatiwa matibabu bure”, amesema Mgombea Urais NRA Mahona.

Aidha ameongeza kuwa atazalisha ajira zisizopungua Milioni 12 kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake ili kuondoa adha ya ajira kwa vijana nchini.

Chanzo Eat Tv

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents