Soka saa 24!

Mkojo wamfanya Pogba kuchelewa ndege, alazimika kurejea na mashabiki wa United kutoka Itali

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amejikuta akichelewa ndege ya kurejea Manchester iliyokuwa imepandwa na wachezaji wenzake kufuatia kuchelewa vipimo vya mkojo mara baada ya mchezo wao wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya klabu ya Juventus.

Paul Pogba (centre) arrives back at Manchester Airport an hour after his team-mates after being kept back for drug testing following Manchester United's 2-1 win over Juventus

Mchezaji huyo raia wa Ufaransa amefika uwanja wa ndege wa Manchester saa moja mbele sambamba na mashabiki akitokea Turin baada ya kuachwa kutokana na kuchelewa huko.

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limekuwalikichagua baadhi ya wachezaji kutoka timu zote mbili na kuchukua sampuli ya mikojo yao kwajili ya kuipima baada ya mechi ikiwa ni njia ya kuzuia kutumika kwa madawa ya yasiyotakiwa michezoni.

Pogba flew back with club executives and fans following the post-match delays in Turin

Katika mchezo huo uliyokuwa na mvuto wa aina yake umeshuhudiwa meneja wa United, Jose Mourinho kurejea nyumbani na furaha baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dakika za lala salama mbele ya kikosi anachokiamini ni bora mno kwa sasa cha Juventus.

Manchester United manager Jose Mourinho was in a happy mood as he arrived back home in the early hours of Thursday morning following their comeback victory

Na mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Manchester Mourinho alipata nafasi ya kusalimiana na Mkurugenzi wa timu hiyo, Ed Woodward.

Licha ya ushindi huo mnono mbele ya Juventus, United sasa itakuwa na kibarua kigumu mbele ya hasimu wake Man City kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza siku ya Jumapili.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW