Michezo

Mkongwe Pele ampa makavu Messi ” Hana uwezo wa kujilinganisha na mimi”

Mkongwe kutoka nchini Brazil aliyezaliwa miaka 78 iliyopita katika jiji la Minas Gerais nchin humo, na kufanikiwa kuvitumikia vilabu viwili tu ambavyo ni klabu kutoka Brazili ya Santos Futebol Clube (Santos) ambapo aliitumikia kuanzia mwaka 1958 – 1974 na kufanikiwa kuifungia magoli 619 kwa michezo 638,pamoja na klabu moja kutoka nchini Marekani ya New York Cosmos (Cosmos) ambapo aliitumikia kuanzia mwaka 1975-1977 na kufanikiwa kuifungia magoli 31 katika michezo 56, vile vile katika timu yake ya taifa alifanikiwa kuichezea michezo 92 na kuifungia magoli 77.lakini pia Pele ndio mchezaji pekee aliyewahi kutwaa taji la kombe la dunia kwa nyakati tatu tofauti.

Mkongwe huyo ameweka wazi na kutoa hisia zake kwa kuwaonywa watu waoamini kuwa mchezaji raia wa Argentina Lionel Messi ndio mchezaji bora wa muda wote dunianiPele alisema:-

” Unawezaje kulinganisha kati ya mchezaji anayeongoza kwa kuuchezea mpira vizuri, anapiga kwa mguu wa kushoto, anatumia pia mguu wa kulia kuuchezea mpira pamoja na viungo vingine vya mwili, halafu umlinganishe na mwingine ambaye hupiga tu mpira kwa mguu mmoja, ana ujuzi mmoja na hata hatumii kichwa kupiga mpira vizuri? “

Pele aliongeza, kulingana na tafsiri ya Folha de Sao Paulo. “Unaweza kulinganishaje? Ili kumlinganisha na Pele, inabidi kuwa na mtu anayepiga na kuuchezea mpira vizuri na miguu yote wa kushoto wa kulia, na mweneye uwezo wa kufunga magoli kupitia kichwa yaani mwenye  alama zote nzuri. “

Hta hivyo Pele hakuishia hapo ni pale baada ya kumuweka Maradona juu ya Messi kwa wachezaji wake 11 bora wa muda wote.

Baada ya kusema “Kama mimi ninaonai, Maradona alikuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani,” alisema. “Ikiwa unaniuliza Maradona alikuwa bora kuliko Messi?’ Jibu langu ni Ndio, Maradona alikuwa bora zaidi kuliko Messi . [Franz] Beckenbauer, na  [John] Cruyff pia walikuwa wachezaji bora zaidi duniani”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents