Burudani

Mkongwe wa Hip Hop Marekani, Prodigy afariki dunia

Rapper kutoka kundi la muziki wa Hip Hop Marekani, Mobb Deep, Prodigy amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 42.

Imedaiwa kuwa mkali huyo alikuwa mjini Las Vegas Jumamosi hii akitumbuiza katika tamasha la ziara ya ‘Art Of Rap’ akiwa na wasanii wenzake kama Ghostface Killah, Onyx, KRS-One, na Ice-T ndipo hali yake ya kiafya ilipokuwa mbaya na kukimbizwa hospitalini.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umeripoti kuwa chanzo cha kifo cha rapper huyo kinatokana na maradhi ya ugonjwa wa Sickle Cell ambao alikuwa amezaliwa nao.

Marehemu Prodigy na rafiki yake Havoc kwa pamoja waliunda kundi la Mobb Deep lililopo mjini New York katika miaka ya 1990.

Hizi ni baadhi ya comment za mastaa mitandaoni kuhusu msiba huo.

Nas: ?? QB RIP King P. Prodigy 4 Ever. Family. We Mobb Deep 4 Ever. RIP PRODIGY

Lil Wayne: Damn. RiP to the great one Prodigy. Rap game lost a legend the world lost a G. ?? to and for his fam. Love. MOBB

Ghostface Killah: Rest In Paradise young Blood @PRODIGYMOBBDEEP can’t believe you gone lord we was just chilling !! Hold ya head @mobbdeephavoc

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents