Burudani

Mkongwe wa muziki Kenya, Pilipili azungumzia kimya chake

Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya kutoka Kenya na vile vile mshindi wa tuzo nyingi za nje na ndani ya nchi, amezungumza kuhusu kuwa kimya na mambo mengine.

Mashabiki waliopenda muziki wake wamekuwa na hamu kubwa ya kutaka kuisikia sauti yake kwakuwa wanamiss uwepo wake kwenye game.

Akizungumza na Pulse , hitmaker huyo wa ‘Iweje’ aliweka kila kitu wazi.

“Muziki ni sehemu kubwa ya maisha yangu so kuacha kufanya muziki ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa. Tuseme nilihisi tu kwamba singeweza kuendelea na kufanya kitu kile kile, aina ile ile ya muziki,”alisema.

“Kwahiyo binafsi niliamua nichukue breki ya muda ili niweze kujifumbua na nijiandae kuja kivingine na nguvu mpya ili niweze kuleta vitu vizuri na vikubwa zaidi kwenye hii game ya muziki. Kwa sasa najihusisha sana na wasanii wapya na chipukizi kwenye game ambapo nawasimamia katika kazi zao kupitia lebo yangu ya Chilli Inc,” aliongeza.

“Nafanya uwekezaji mzuri kwa sababu kinachokuja sio cha kawaida tena. Napania kurudi na audios pamoja na videos kali kali.”

Pilipili ameahidi makubwa na amewataka mashabiki wa muziki wake kutoka kila sehemu wawe tayari kwa ujio wake mpya.

Pilipili aliwahi kusumbua spika zetu kipindi cha nyuma kupitia hit songs kama ‘Mpaka Chee’ , ‘Iweje’, ‘Wanipimia’ na nyingine

Na: Teddyza Agwa
Insta: @teddyzabway
+254710487436
Chanzo: pulse(Kenya)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents