Tragedy

Mkongwe wa muziki wa dansi Mzee Kassim Mapili afariki dunia

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Kassim Mapili amefariki dunia.

image1
Mzee Kassim Mapili (kulia) akiwa na rais wa shirikisho la muziki Tanzania, Ado November

Mzee Mapili alikutwa amefariki nyumbani kwake Tabata Matumbi. Inasemekama kifo chake kimejulikana usiku wa jana baada ya majirani kutomuona siku mbili nzima na kutia mashaka, ndipo walipoamua kuvunja mlango wa nyumba yake na kukuta mwili wake.

Majirani wa Mzee Mapili wamesema mara ya mwisho kumuona mkongwe huyo ambaye alikuwa akiishi peke yake nyumbani kwake, ni juzi ambapo waliangalia pamoja mtanange kati ya tinu za Arsenal na Barcelona.

Shuhuda mmojawapo amesema mwili hauko katika hali nzuri, na jitihada za kuwatafuta ndugu zake zinaendelea. Mzee Mapili alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Moyo kabla ya kifo chake.

Taarifa kutoka kwa Rais wa shirikisho la muziki nchini, Ado November imesema:

Nimepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa za Kifo cha Mzee wetu Mzee Mapili. Atakumbukwa kwa kibao cha ‘Napenda Nipate Lau Nafasi na Rangi ya Chungwa. Mazishi ya leo Ijumaa 26/02/2016 saa kumi jioni Kisutu. Maiti haipo ktk hali nzuri daktari kashauri azikwe haraka. Msiba upo mtaa wa Magomeni na.23 Mapipa. Tujitokezeni wapendwa kama ungependa kujiunga nasi kwa mchango basi tuma rambirambi kwa Hassan Msumari-Katibu Mkuu Chamudata, namba zake 0717340533, Addo November – Rais Shirikisho la muziki Tanzania – 0744150000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents