Tupo Nawe

Mkono wa Mkonole, Kiwewe na Matumani kuachia wimbo wa pamoja wa gospel comedy ‘Nimepona’

Msanii wa vichekesho Mkono wa Mkonole anatarajia kuachia wimbo wa gospel comedy uitwao ‘Nimepona’ alioimba na wachekeshaji wenzie, Kiwewe na Matumaini ili kutoa burudani ya uchekeshaji sambamba na kumuabudu Mungu.

page

Ujio wa wasanii hao na wimbo wa ‘Nimepona’ umekuja baada ya wasanii hao kujadiliana na kugundua pia kupitia uchekeshaji wanaweza kumshukuru Mungu kwa kupitia kipaji cha uchekeshaji ambacho wamepewa na Mungu na pia kuonyesha ni jinsi gani wanaweza kuitumia sanaa yao kufikisha ujumbe kwa jamii.

“Sisi ni wasanii na ni kioo cha jamii kwahiyo tunapenda kuwajulisha ndugu watanzania, wapenzi wa burudani pamoja na wadau wote wa muziki wa injili kuwa mkae tayari kwa kupokea nyimbo mpya inayoitwa Nimepona ambayo imeandaliwa kutoka katika kundi la ‘Comedian Gospel’ linaloundwa na Mkono wa Mkonole, Kiwewe na Matumaini, Mkono wa Mkonole aliambia Bongo5.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW