Michezo

Mkude awaomba Watanzania kwa hili ‘Sisi ni Tanzania, sisi ni Taifa Stars, kwa pamoja tuungane’

Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas MKude ameungana na Watanzania katika kuhakikisha wanaisapoti timu ya taifa  ‘Taifa Stars’ ambayo inakibarua kizito cha kuibuka na pointi tatu muhimu dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ hii leo.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram, Mkude ameandika kuwa kama Watanzania kwa pamoja tuungane kuwaombea wawakilishi wetu.

”Sisi ni Tanzania. Sisi ni Taifa Stars. Kwa pamoja, tuungane kuwaombea wawakilishi wetu kwenye mchezo wa leo dhidi ya Uganda,” ameandika Mkude.

Stas ikiwa chini ya nahodha mahiri Mbwana Samatta itashuka dimbani hii leo majira ya saa 10 alasiri kuikabili timu ya taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2019.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents