Mkulo atoa tamko wastaafu EAC

SERIKALI imetoa wito kwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukubali malipo yaliyolipwa baada ya uhakiki kuwa ni halali. Kauli hiyo ya serikali ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Fedha na Uchumi

SERIKALI imetoa wito kwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukubali malipo yaliyolipwa baada ya uhakiki kuwa ni halali.

Kauli hiyo ya serikali ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Fedha na Uchumi na kusema kuwa malipo hayo yamefanywa kutokana na hati ya makubaliano ya mahakama.

“Serikali inawasihi wazee hao, kujiepusha na upotoshaji na udanganyifu wa wajanja wachache wanaojinufaisha kupitia migongoni mwao kwa visingizio vya kuendelea kusimamia madai ambayo hayapo,” alisema Waziri Mkulo.

Alisema kwa mujibu wa hati hiyo ya makubalino hadi Septemba 30, mwaka huu, serikali ilikuwa imeshawalipa wastaafu 31,444 sh bilioni 114.

Aidha, Waziri Mkulo alisema malipo hayo yamefanyika kwa misingi ya haki na sheria, kwani yamezingatia hati ya makubaliano iliyohitimishwa na mahakama, kanuni na taratibu za nchi.

Alisema kuwa kwa sasa hakuna malipo mengine nje ya hati ya makubaliano hayo na kuongeza kuwa kutokana na matatizo yanayoweza kujitokeza kwa mtu mmoja mmoja kama ilivyojitokeza katika zoezi la Septemba mwaka huu, wizara yake itaendelea kupokea maombi ya aina hiyo kutoka kwa wastaafu halali na kuyashughulikia ipasavyo.

“Kwa mfano kati ya wastaafu 21 waliodhihirika kuwa wanastahili kulipwa, wastaafu 10 hundi zao ziko tayari na wanaweza kuzichukua wakati wowote, Hazina, Dar es Salaam,” alisema Mkulo.

Awali, alisema katika kutekeleza jukumu la kuwalipa wastaafu hao, matatizo mbalimbali yalijitokeza, ikiwa ni upungufu wa nyaraka ambao umechelewesha zoezi hilo kuweza kukamilika mapema.

Aliyataja matatizo hayo kuwa ni madai yasiyo na ushahidi, madai ya wafanyakazi wasiohusika wala kustahili malipo yoyote kama vile walioajiriwa baada ya kuvunjika kwa jumuiya hiyo Juni 30, 1977.

Matatizo mengine ni waliostaafu kabla ya jumuiya kuvunjika, waliokuwa vibarua wa Cargo, wafanyakazi wa iliyokuwa Bora shoes, wafanyakazi wa iliyokuwa East African Breweries na wafanyakazi wa iliyokuwa UDA.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents