Burudani

Mkurugenzi wa Candy and Candy, Joe mbaroni Arusha

Hali ya bosi wa kampuni ya sanaa ya Candy and Candy Joe Kairuki inadaiwa kuwa mbaya ambapo amelazwa katika hospitali moja iliyopo Longido mkoani Arusha akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Mkurugenzi wa Candy and Candy, Joe (katikati) akiwa na baadhi ya wasanii wake wa zamani.

Joe ambaye ni raia wa Kenya, amewahi kuwa meneja wa wasanii maarufu nchini, Mr. Nice, Top C, Baby Madaha na ni mmiliki wa mtandao wa Nikohub akiwa ni mshika dau wa gazeti la Bab Kubwa.

Amewahi kuingia katika mahusiano na mwanamuziki wa kike Bongo, Baby Madaha aliyeimba ngoma ya Amore.

Inaelezwa kuwa Joe ambaye hufanya biashara zake hapa nchini ambapo amefungua tawi la Candy and Candy kwa lengo la kuwekeza katika filamu, muziki na matamasha, alikamatwa juzi na jeshi la polisi wilayani Longido kwa tuhuma za kumtaperi mfanyabiashara Yusuf Mohamed raia wa Kenya kiasi cha sh.milioni 300.

Kwa mujibu wa mwanasheria wake John Malya, alisema Joe alikamatwa juzi baada ya kesi yake ya awali kutupiliwa mbali na mahakama ya Arusha, kisha kukamatwa tena nje ya mahakama.

Inaelezwa kuwa awali Joe alikamatwa Julai 2 mwaka huu na kutupwa lumande huku kukiwa hakuna ndugu wala rafiki aliyekuwa anafahamu alipo.

“Baada ya kufikishwa mahakamani shauri lake lilifutwa juzi kisha polisi walimkamata nje ya mahakama na kumpeleka kituo cha polisi Longido ambako anashikiliwa,”alisema Malya.

Alisema alipohojiana na Polisi walimwambia kuwa atapelekwa mahakamani tena jumatatu na kuunganishwa na mtuhumiwa mwingine katika kesi iliyokuwa imefutwa ambayo itafunguliwa upya.

Malya alisema hali ya Joe ilibadilika ghafla kutokana na kukosa chakula hivyo kulazimika kulzwa hospitali huku akiwa katika hali mbaya.

Mwanasheria huyo alisema wamepanga shauri la Joe kulifikisha Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ili kesi hiyo iweze kuhamishiwa nchini Kenya ambako mdai na mtuhumiwa ni raia wa huko na fedha wanazodaiana walipeana wakiwa nchini humo.

Mmoja wa watu wa karibu wa Joe aliwataka wadau kujitokeza kumsaidia Joe kwani hali yake ya afya si njema na pia amekosa msaada wa karibu.

Jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha zinaendelea…

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents