Siasa

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam atoa onyo kali kuelekea uchaguzi, mtu asijaribu kuleta fujo tumejipanga (+Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa onyo kali kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya fujo siku ya uchaguzi ambapo ameeleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na usalama.

RC Kunenge ametoa onyo hilo wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ambapo ametoa wito kwa wananchi wote waliojiandikisha kutumia haki yao ya msingi kwa kutijokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka.

Aidha RC Kunenge ameeleza kuwa hali ya amani na utulivu kwenye jiji hilo ni shwari na utaendelea kuwa shwari siku zote hivyo hakuna sababu yoyote ya wananchi kuwa na wasiwasi.

Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa ngazi ya Urais, Wabunge na Madiwani utafanyika October 28 ambapo Rais Dkt. John Magufuli amepanga siku hiyo kuwa ya mapumziko ili kila mwananchi aweze kupata nafasi ya kutumia haki yake ya msingi ya kupiga kura.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents