Habari

Mkuu wa polisi wa Venezuela matatani kwa matumizi mabaya ya nguvu kwa waandamanaji

By  | 

Mkuu wa zamani wa jeshi la polisi nchini Vanezuela, Antonio Benavides anatarajia kuhojiwa kutokana na kutumia vibaya madaraka yake kwa raia waliokuwa wakiandamana kuipinga serikali iliyopo madarakani.


Picha ya Antonio Benavides akiongea na waandishi wa habari

Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa nchi hiyo imemtaka kiongozi huyo wa polisi kutoa maelezo ya unyanyasaji huo kwa raia wake.

Benavides ambaye aliondolewa katika nafasi yake hiyo wiki iiyopita, anatarajiwa kuanza kufanyiwa mahojiano hayo wiki ijayo ya Julai 6.


Hali ilivyokuwa wakati wa maandamano nchini Venezuela

Zaidi ya watu 80 wanadaiwa kuuawa na jeshi la pplisi la Venezuela wakati wa maandamano yaliyodumu takribani miezi mitatu ya kupinga utawala wa Rais Nicolas Maduro.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments