Michezo

Mkuu wa riadha Kenya asimamishwa kwa miezi 6

Mkurugenzi mkuu wa shirikisho la riadha la Kenya bwana Isaac Mwangi amepigwa marufuku na shirikisho la riadha duniani IAAF, kwa siku 180.

160222171651_isaac_mwangi_624x351_kwahisani

Bwana Mwangi anatuhumiwa kwa kuwaitisha hongo wanariadha wawili waliopatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini ilikupunguza kipindi cha marufuku yao.

Mwangi amekanusha madai dhidi yake.

Mkurugenzi huyo mkuu tayari amejiondoa kwa siku 21 ilikufanikisha uchunguzi dhidi yake.

Kufuatia marufuku hii yakamati ya maadili basi bwana Mwangi hatakuwa na mchango wowote katika mashindano ya olimpiki yatakayofanyika mjini Rio Brazil mwaka huu.

Kupitia kwa taarifa maalum mkuu wa kamati ya maadili bwana Michael Beloff QC amepigwa marufuku kwa kujaribu kuhujumu kampeini dhidi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini.

Marufuku yake inaanza mara moja yaani kuanzia tarehe 22 mwezi Februari 2016.

Mkurugenzi huyo alijipata matatani baada ya wanariadha wawili Joy Sakari na Francisca Koki Manunga kudai kuwa Mwangi alikuwa amewaitisha hongo ya takriban dola elfu hamsini ilikupunguza kipindi cha marufuku.

Joy Sakari na Francisca Koki Manunga walipatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini katika mashindano ya riadha duniani yaliyofanyika huko Beijing Uchina.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents