Mkuu wa shule, Afisa Elimu wapewa siku tatu na Naibu Waziri Silinde (+Video)

Naibu waziri wa TAMISEMI  Mhe. David Silinde ametoa siku tatu kwa Mkuu wa shule ya msingi  Katesh A na Afisa Elimu msingi wa wilaya hiyo kupeleka taarifa za kwanini ujenzi wa mabweni katika shule ya msingi Katesh A  ya wanye mahitaji maalum katika wilaya ya Hanang mkoa wa Manyara haujakamilika kwa zaidi ya miezi sita ikiwa hela zote zimetolewa toka Juni,2020 kupitia mradi wa lipa kulingana na  matokeo (EP4R) na kwanini wasichukulie hatua za kinidhamu kwa kuchelewesha mradi huo.

Mhe. silinde amechukua uamuzi huo baada ya kutembelea ujenzi wa mabweni wa shule hiyo na kukuta ujenzi huo haujakamilika na fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi zikiwa zimebadilishiwa matumizi bila kuomba idhini ya OR-TAMISEMI ya kuzitumia fedha hizo kumalizia jengo lilojengwa kwa nguvu za wananchi na fedha zilizobaki kujenga bweni moja.

Naibu Waziri Silinde  hakuridhishwa na sababu hizo zilizotolewa na mwalimu mkuu wa shule hiyo na kusema majengo wanayoishi wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu hayaendani kabisa na hadhi na utu wa binadamu kwa kua machakavu sana.

“Nia ya Mhe. Rais watoto wenye mahitaji Maalum wapate sehemu nzuri ya kukaa na kuwa ma malazi bora na haya majengo ya zamani wanayokaa ni kama yale majengo ya ‘escape from sobibo’  hayaendani na hadhi ya binadamu haswa kwa watoto mwenye mahitaji maalum kukaa mule ndani ni kama wapo katika kifungo”

Naibu waziri Silinde ameagiza majengo hayo yakamilike haraka na mwisho wa mwezi huu wanafunzi hao waweze kuyatumia kuliko kuendelea kukaa kwenye kmajengo ya zamani.

Aidha Naibu Waziiri ameagiza uongozi wa  halmashauri waandike barua kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuchelewesha ujenzi huo na ndani ya siku 14 wapeleke taarifa TAMISEMI za maendeleo ya ujenzi wa shule zote mpya zinajengwa katika maeneo yao na hali ilipofikia hii ni kutokana na kwamba fedha zimetolewa lakini ujenzi bado unasusua.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW