Burudani ya Michezo Live

Mkuu wa Wilaya Bariadi, Kiswaga alivyopokea neema ya Tigo kwa Wananchi wake

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mh.Festo Kiswaga amezipongeza juhudi za Tigo katika kuwekeza rasilimali katika uboreshaji wa huduma na kuhakikisha zinakidhi viwango vya kimataifa. Hayo yamejiri wakati kampuni hiyo ikizindua duka lao jipya Wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga(aliyevaa shati la kitenge) akikata keki sambamba na wateja wa tigo wakati wa hafla ya uzinduzi wa dula la Tigo katika mtaa wa Sokoni mkoani Simiyu.

“Huduma bora kwa wateja ni kitovu cha biashara na zaidi huwafanya wateja wajisikie wanathaminika na kuheshimiwa, Tigo wametekeleza jambo hili kwa vitendo kwa kufanya uwekezaji katika utoaji wa huduma zao jambo linalowapa utofauti wa kipekee sokoni,” alisema Lalika.

Kampuni hiyo inayoongoza katika maisha ya kidijitali  Tanzania, imefungua duka jipya jijini Bariadi. Duka hilo litawafanya wateja wa kampuni hiyo kupata huduma zote kwa urahisi zaidi ndani ya eneo moja.

Duka hilo litatoa huduma zote muhimu kuanzia usajili wa namba za simu kwa alama za vidole, huduma za kifedha ‘Tigo Pesa’ na mauzo ya data na vifaa vya mawasiliano kama simu janja, router na modem kwaajili ya huduma yetu ya Tigo Home interne

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati amesema hatua ya kufungua duka hilo ni moja ya mkakati wa Tigo wa uboreshaji wa huduma na kuhakikisha zinawafikia wateja kwa wakati nchi nzima.

“Duka hili jipya litampa mteja wetu wasaa wa kutazama na kujaribu bidhaa mbalimbali kabla ya kuamua kufanya manunuzi.Hatua hii imekuja kufuatia maombi ya muda mrefu kutoka kwa wateja wetu waliokuwa wakihitaji uwepo wa duka letu kwenye jengo hili maarufu kibiashara hivyo tumekidhi mahitaji yao,”alisema Madati.

“Huduma bora kwa wateja ni kitovu cha biashara na zaidi huwafanya wateja wajisikie wanathaminika na kuheshimiwa, Tigo wametekeleza jambo hili kwa vitendo kwa kufanya uwekezaji katika utoaji wa huduma zao jambo linalowapa utofauti wa kipekee sokoni,” alisema Lalika.

Kadhalika,duka hilo linakuwa la nne kufunguliwa mkoani humo huku likiwa na huduma mpya ikiwamo simu zinazotamba kwa sasa aina ya Kitochi 4G Smart pamoja na vifaa vya huduma za intaneti kwa makampuni maarufu kama ‘Tigo business’.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW