Michezo

Mkwasa acharuka Manara kuiwakilisha Yanga aitisha kikao cha dharura

Uongozi wa Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga umeonyesha kutofurahishwa na kitendo cha kutoalikwa katika hafla ya ukabidhi wa vifaa iliyofanywa na wadhamini wa Ligi Kuu Bara, kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.

Wakati wa ukabiziwaji wa vifaa hivyo kwa timu mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi wa idara ya masoko na usambazaji Vodacom, Hisham Hendi yanga imeonekana kutokuwa na muakili na kupelekea Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara kujitokeza kwa niaba ya mabingwa hao wa ligi kuu.

Vodacom imekabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 500 ambavyo ni pamoja na jezi za mazoezi na zile za mechi kwa timu zote 16 zitakazocheza ligi hiyo msimu ujao.

Katibu Mkuu wa Yanga SC, Boniface Mkwasa amesema wamesikitishwa na jambo hilo na hasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents