Michezo

Mkwasa ndio kocha mpya Taifa Stars

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi amemtangaza Boniface Mkwasa kama kocha mpya wa Taifa Stars.

Boniface-Mkwasa

Mkwasa anachukua nafasi ya mholanzi Mart Nooij aliyeagwa Jumanne hii baada ya mkataba wake kusitishwa.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema wameamua kuagana na Nooij mbele ya vyombo vya habari kama iliyofanyika pia wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi.

Jamal Malinzi pia amemtangaza Hemed Morocco kama kocha msaidizi.

Chanzo: tff.or.tz

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents