Burudani ya Michezo Live

Mlandizi: Ajali iliyosababishwa na magari manne kugongana likiwemo lori yapelekea kifo mtu mmoja na majeruhi

Gari nne likiwemo lori la mafuta zimegongana na kusababisha ajali katika eneo la Mlandizi mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo Julai 2, na kupelekea kifo cha mtu mmoja na majeruhi watatu, abiria wanaotokea Dar es Salaam wameshauriwa kutumia barabara ya Bagamoyo.

“Julai Mosi, 2020 saa 5 Usiku eneo la daraja la Mkalamo, imetokea ajali ya magari manne kugongana na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi watatu. Mawili yalikuwa na shehena ya mafuta, moja lenye shehena ya viazi na lenye simenti”- Kamanda Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa.

“Majeruhi wapo katika hospitali ya Tumbi pamoja na mwili wa marehemu lakini ninawashauri wasafiri wanaotokea Dar es Salaam watumie barabara ya Bagamoyo ili tuweze kuifungua hii barabara kwa sababu foleni ni kubwa sana” – Kamanda Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa.

Chanzo Eatv.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW