Shinda na SIM Account

Mlemavu maarufu duniani apata watoto mapacha

Msemaji maarufu duniani raia wa Australia mwenye ushawishi mkubwa ambaye pia amezaliwa akiwa na ulemavu wa mikono na miguu, Nicholas James Vujicic amefanikiwa kupata watoto mapacha.

Nicholas na mkewe Kanae Vijicic wamefanikiwa kupata watoto hao mapacha wawili Jumatano ya wiki hii.


Olivia Mei (aliyefungwa kikamba chekundu) na Ellie Laurel (aliyefungwa kikamba cha njano).

Vujicic amethibitisha hilo kupitia mtandao wa Facebook kwa kuandika, “Our Identical Double Blessing from Our Gracious and Almighty God! Born Dec 20th – Olivia Mei Vujicic (red bow, 5lbs2oz @ 7:54am) and Ellie Laurel Vujicic (yellow bow, 5lbs14oz @ 7:56am) !!! Mommy (Kanae Vujicic) and Girls doing wonderful.

Tayari watoto hao ambao wote ni wakike wamepewa majina ya Olivia Mei na Ellie Laurel. Mpaka sasa Vujicic atakuwa na watoto wanne akiwemo Kiyoshi James (4) na Dejan Vujicic (2) na hao mapacha .

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW