Habari

Mlimani hakukaliki

Licha ya Chuo Kikuu Dar kufunguliwa jana na wanafunzi wa shahada ya kwanza kuripoti huku mamia wakihangaika kujaza fomu maalum za kurejea kwao, bado chuo hicho sehemu ya Mlimani hakukaliki kwa amani kutokana na hofu waliyonayo wanafunzi.

Na Mwandishi Wa Alasiri, Jijini



Licha ya Chuo Kikuu Dar kufunguliwa jana na wanafunzi wa shahada ya kwanza kuripoti huku mamia wakihangaika kujaza fomu maalum za kurejea kwao, bado chuo hicho sehemu ya Mlimani hakukaliki kwa amani kutokana na hofu waliyonayo wanafunzi.


Hofu hiyo inatokana na taratibu kibao zilizotangazwa katika kurejea huko na tishio la mgomo mwingine lililotangazwa jana.


Kwa mujibu wa baadhi ya wanafunzi waliozungumza na mwandishi wa gazeti hili, ni kwamba sharti la kujaza fomu maalum kwa wale walioshindwa kulipia asilimia arobaini ya gharama za masomo yao na kitendo cha kusimamishwa kwa viongozi kibao wa Serikali ya Wanachuo, DARUSO, ni baadhi ya mambo yanayowafanya wajawe na hofun juu ya musktakabali wao kimasomo.


Hofu zaidi kwa maelfu ya wanafunzi wa shahada ya kwanza waliokuwa wamesimamishwa tangu April 18 mwaka huu, ni juu ya uamuzi wa chuo katika kuwasimamisha masomo wenzao 56 kwa madai kwamba ndio waliokuwa waanzilishi wa mgomo.


Zinasema taarifa hizo kuwa jana, baada ya Bunge la Serikali ya wanafunzi kukutana na kujadili hatma ya kusimamishwa kwa wenzao 56 ambao karibu wote ni viongozi wa DARUSO, imeamuriwa kwamba baada ya siku mbili kupita, kutaitishwa mgomo mwingine wa kutaka nao waruhusiwe kuendelea na masomo.


Aidha, taarifa hizo zinasema kuwa kwa mujibu wa maazimio ya bunge la chuo hicho lililokaa jana katika ukumbi wa Art Theatre B (ATB), ni kwamba hatua itakayofuata ni kuwasiliana na wanasheria ili kukiburuza chuo kortini.


�Hali hiyo ya tishio la mgomo na haya mafomu tunayolazimishwa kuyajaza huku tukiapa kwa wanasheria ni baadhi ya mambo yanayofanya chuo kwa sasa kisikalike kwa amani,� amesema mmoja wa wanafunzi wa shahada ya kwanza chuoni hapo kuiambia Alasiri leo asubuhi.


Katikati ya mwezi uliopita, wanafunzi wa Chuo hicho waligoma kwa siku mbili wakipinga kutakiwa walipie asilimia arobaini ya ada na gharama nyingine za masomo yao, kwa madai kwamba wengi wanatoka familia maskini na wazazi wao, kamwe hawana uwezo wa kulipia gharama hizo.


Kwa sababu hiyo, uongozi wa chuo ukawasimamisha masomo wanafunzi wote wa shahada ya kwanza na kuwapa masharti kadhaa kabla kuwaruhusu kurejea chuoni jana, huku ikiwasimamisha wengine 56 kwa madai kwamba ndio walioongoza mgomo huo.


Source: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents