Michezo

Mlindalango wa Manchester United apata ajali mbaya ya gari

Mlindalango wa klabu ya Manchester United, Sergio Romero amepata ajali ya gari wakati akielekea kwenye kiwanja cha mazoezi cha Carrington.

Image result for MANCHESTER UNITED ace Sergio Romero has been involved in a horror car crash.

Sergio Romero mwenye umri wa miaka 32, amepata ajali hiyo akiwa katika gari lake jeupe aina ya Lamborghini lenye thamani ya paundi, 170,000 ambayo sawa na shilingi milioni 510 za Kitanzania.

Hata hivyo taarira zinasema kuwa golikipa huyo mzaliwa wa Argentina hajapata majeraha kwenye ajali hiyo. Romero alijiunga na Manchester United mwaka 2015 akitokea klabu ya Sampdoria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents