Fahamu

Mlipuko wa Virusi vipya vyasambaa kwa kasi China, Rais Xi Jinping atoa tahadhari

Mlipuko wa virusi vipya vinavyouwa vinasambaa kwa kasi, Rais Xi Jinping ametoa tahadhari baada ya kufanya kikao maalum katika siku ya mwaka mpya wa Lunar.

People wear protective masks as they walk outside a shopping mall in Beijing on January 23

Rais aliwaambia maofisa wa ngazi za juu kuwa nchi iko kwenye hali ya hatari kubwa , kwa mujibu wa televisheni ya taifa.

Virusi vya corona tayari vimeuwa watu wapatao 41 na wengine 1,400 wameambukizwa tangu virusi hivyo vigundulike huko Wuhan.

Tayari miji mingi imeweka katazo la kusafiri kwa watu wake.

Na siku ya jumapili hata magari binafsi hayataruhusiwa kutoka Wuhan, eneo ambalo virusi hivyo viibainika kwa kwa mara ya kwanza.

Hospitali nyingine ya dharura inajengwa na inategemewa kuwa ndani ya wiki , itaweza kuwahudumia wagonjwa wapya 1,300, na itamalizika kujengwa ndani ya nusu mwezi, gazeti la serikali la la People’s Daily limeripoti.

Huu ni mradi wa pili wa ujenzi wa hospitali ambao unafanyika, hospitali nyingine ujenzi wake umeanza tayari na inategemea kuchukua wagonjwa 1000.

Kikosi maalum cha wanajeshi ambao ni madaktari tayari wameenda jimbo la Hubei , eneo ambalo Wuhan ipo.

Angalizo la virus hivi lilitolewa kwa China na maeneo mengine duniani tangu mwezi Desemba, wakati virusi hivyo vilipogundulika..

Sherehe za mwaka mpya wa China ambao mwaka huu ni wa panya zilianza siku ya jumamosi, lakini tafrija za sherehe hizo zilisitishwa kufanyika katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

wanapimwa homaHaki milikiĀ 

Mpakani wasafiri wamekuwa wakipimwa joto lao kuangaliwa kama wana hali yoyote ya homa na usafiri wa tren umefungwa pia katika miji kadhaa.

Huko Hong Kong, taarifa ya dharura imeongeza muda wa likizo wa shule .

Nchi kadhaa nyingine zimeanza kutibia wagonjwa wake kwa uangalizi wa peke yake.

Virusi vya corona vilianza lini?

Virusi hivi havijawahi kutokea kabla ya mwezi desemba mwaka 2019 na vikapewa jina la “novel coronavirus”.

Virusi vya aina hii huwa kwa kawaida vinawaathiri wanyama lakini mara nyingine, vinaweza kuwapata binadamu, kwa mfano mlipuko wa ugonjwa wa ‘Sars’ ambao uliuwa watu wengi China.

In Hong Kong's Wong Tai Sin temple, people welcome the new year in masks

Virusi vya coronaus, awali vilikuwa havijatambuliwa na wanasayansi, huwa vinamfanya mtu mwenye maambukizi kuwa na dalili za homa na kikohoa.

Hakuna tiba wala chanjo inayoweza kuzuia maambukizi hayo mpaka sasa.

China yote ikoje?

china

Maafisa wa mji mkuu wa Beijing, na Shanghai wamewataka watu wanaotoka katika maeneo yenye maambukizi kubaki nyumbani kwa muda wa siku 14.

Mamlaka imefunga maeneo yote ya utalii likiwemo eneo la Forbidden mjini Beijing pamoja na upande wa Great Wall, Matukio ya umma yamesitishwa pia katika maeneo yote ya nchi ikiwa pamoja na :

Huduma za kitamaduni za kwenye mahekalu Beijing. Tamasha la kimataifa la Hong Kong Mashindano ya mwaka ya mpira wa mguu Hong Kong , Sherehe zote za mwaka mkpya wa China huo Macau

Mgahawa wa McDonald umeripotiwa kufungwa katika miji mitano. Siku ya alhamisi mgonjwa wa corona alifariki kaskazini mwa jimbo la Hebei – na hicho kuwa kifo cha kwanza kutangazwa nje ya mji wa Hubei.

Vifo vingine vilithibitishwa kutokea baadae kaskazini-mashariki mwa jimbo la Heilongjiang, zaidi ya kilomita 2000 kutoka mji wa Wuhan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents