Burudani ya Michezo Live

Mlipuko walikumba basi la timu ya Borussia Dortmund na kusababisha kuahirishwa mechi ya robo fainali mabingwa wa Ulaya dhidi ya Monaco

Milipuko miwili imelikumba basi la timu ya Borussia Dortmund iliyokuwa ikielekea kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Monaco.

Akaunti ya Twitter ya timu hiyo imethibitisha tukio hilo lilitokea wakati timu ikitoka kwenye hoteli ya L’Arrivee iliyopo maili mbili tu toka uwanja wa Signal Iduna Park wa mjini Dortmund, Ujerumani.

Beki Marc Bartra amejeruhiwa kwenye mlipuko huo na amepelekwa hospitali.

Mchezo huo uliokuwa uchezwe leo usiku, umeahirishwa hadi kesho. Chanzo cha mlipuko huo bado hakijulikani.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW