Marimba Music Chart

MMC: Lady JayDee, BenPol watoka, Vanessa Mdee, Damian Soul waingia katika Marimba Music Chart wiki hii (28th November 2013)

Wiki hii jumla ya nyimbo nne zimeiaga chart ya Marimba na nafasi zake kuchukuliwa na nyimbo zingine nne zilizoingia. Nyimbo hizo ni pamoja na ‘Yahaya’ ya Lady JayDee pamoja na ‘Jikubali’ ya Ben Pol zilizodumu katika chart za Marimba kwa takriban majuma 18 kila moja.

Vanessa Come Over

Nyimbo zingine zilizotoka ni ‘My Baby’ ya Quick Racka iliyokaa wiki 17, pamoja na ‘Jana na Leo’ ya Young Killer na Stamina iliyokaa wiki 18.

Nyimbo mpya zilizoingia kwenye chart wiki hii ni pamoja na ‘Come Over’ ya Vanessa Mdee, ‘Ni Penzi’ ya Damian Soul , ‘Basi Njoo Kariakoo’ ya Abby Skills pamoja na’ Mdudu’ ya Solo Thang.

Marimba Music Chart (MMC) ni chart rasmi ya muziki wa kizazi kipya Tanzania, ambayo huandaliwa na BONGO 5 kila wiki kutokana na Chart za Radio mbalimbali (zinazowakilisha radio zote) Tanzania.

HII NDIO CHART RASMI YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA WIKI HII (28th November 2013)
MARIMBA CHART (28th NOV 2013)-1
MARIMBA CHART (28th NOV 2013)-2

Ingia HAPA kupata chart ya Marimba ya wiki iliyopita (21st November 2013)

VYANZO:
MARIMBA CHART SOURCES (14th NOV 2013)

VIGEZO:
MMC inatumia Chart za radio mbalimbali za Tanzania (sample) kuchuja na kupata orodha ya nyimbo zilizoingia katika chart nyingi zaidi na kupata nyimbo 20 ambazo ndio zinazofikia kigezo cha kuingia katika Marimba Music Chart.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents