Marimba Music Chart

MMC: Ommy Dimpoz ampiku Lady JayDee na kukaa kileleni baada ya ‘Yahaya’ kutawala kwa wiki 10 katika Marimba Music Chart (03rd October 2013)

Baada ya kutawala nafasi ya kwanza kwa wiki 10 mfululizo hatimaye ‘Yahaya’ ya Lady JayDee imeenguliwa katika nafasi hiyo na hit song ya Ommy Dimpoz ‘Tupogo’ yenye takribani wiki 8 kwenye chart za Marimba. Kabla ya kukwea kileleni ‘Tupogo’ wiki iliyopita ilikamata nafasi nafasi ya 8.

Ommy dimpoz-2

Hii ni wiki ya 11 ya chart rasmi ya muziki wa kizazi kipya Tanzania ‘Marimba Music Chart’, inayotokana na chart za radio mbalimbali za Tanzania. Wiki hii kuna mabadiliko makubwa katika chrt hizi , ambapo nyimbo nyingi zimebadilishana nafasi kwa kupanda na kushuka.

Marimba Music Chart (MMC) huandaliwa na BONGO 5 kila wiki kutokana na Chart za Radio mbalimbali (zinazowakilisha radio zote) Tanzania.

HII NDIO CHART RASMI YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA WIKI HII (03rd October 2013)

MARIMBA CHART (03RD OCT 2013)-1
MARIMBA CHART (03RD OCT 2013)-2

Ingia HAPA kupata chart ya Marimba ya wiki iliyopita (26th Sept 2013)

VYANZO:
MARIMBA CHART SOURCES (03rd OCT 2013)

VIGEZO:
MMC inatumia Chart za radio mbalimbali za Tanzania (sample) kuchuja na kupata orodha ya nyimbo zilizoingia katika chart nyingi zaidi na kupata nyimbo 20 ambazo ndio zinazofikia kigezo cha kuingia katika Marimba Music Chart.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents