Michezo

Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi kuwania urais wa DRC

Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi ametangaza kuwa atawania urais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mwaka huu.

87807062ea9b6bb743a805380118fe99

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Tajiri huyo aliyewahi kuwa gavana wa jimbo la Katanga tangia mwaka 2007 hadi Septemba mwaka jana, atawania urais kupitia muunganiko wa vyama vitatu vidogo vya upinzani. Bado hajaungwa mkono na vyama vikubwa vya upinzani.

Rais wa sasa, Joseph Kabila anamaliza muhula wake wa pili lakini wapinzani wanadai kuwa huenda akataka kuendelea kubaki madarakani kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imedai kuwa uchaguzi utachelewa kufanyika katakana na ukata.

Umiliki wa klabu maarufu ya TP Mazembe iliyochukua ubingwa wa michuano ya mabingwa Afrika umemfanya awe maarufu nchini humo.

Alijiondoa kwenye chama tawala, People’s Party na kuhamia Reconstruction and Democracy,.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents