Burudani

Mmiliki wa Tongwe Records J-Murder: Hatujui Roma na wenzake walipo

Wasanii watatu ambao ni Roma, Monii Central Zone, Bin Laden pamoja na Imma ambaye ni mfanyakazi wa Mama mzazi wa mmiliki wa studio za Tongwe Records J Murder, mpaka muda huu hawajaweza kupatikana na haifahamiki wapi walipo baada ya kuvamiwa studio na kuchukuliwa na watu wasiojulikana.

Muda mchache, J Murder ameeleza kiundani juu ya tukio hilo ambalo binafsi anadai limemshtua sana, wakati akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo kupitia kipindi cha The Splash kinachoruka redio Ebony FM.

“Sijui kisa ni nini kusema ukweli kwa sababu mimi studio sikuwepo ila kitu ninachojua mimi ni kwamba walikuja watu pale na gari aina ya Noah wakamhoji Roma baada ya hapo wakawahoji na watu wengine halafu nasikia wakaingia studio nakujukua baadhi ya vifaa” amesema J Murder.

“Baada ya hapo wakaondoka na wasanii wangu, amechukuliwa Roma, Monii, Bin Laden pamoja na mfanyakazi wa mama angu anaitwa Imma, mpaka sasa hivi hatujui wako wapi namba zao zinaita lakini hazipokelewi wakati wakivamiwa kulikuwa hakuna ulinzi walikuwepo wasanii hao na majirani ambao ni mashabiki wa studio,” ameongeza J Murder.

Mapema leo Mmiliki hiyo wa Tongwe Records alifika kituo cha Polisi Osterbay na anaendelea kutujuza kilichomfikisha pale. “Jana usiku baada ya kutokea tukio nilienda kutoa ripoti pale polisi Osterbay kwahiyo leo nilichoenda pale ni kujua mpelelezi wa kesi yangu ni nani nimpe maelekezo wa vitu gani vime-happen pale studio.”

“Nachowaambia mashabiki wa Tongwe, kwamba tuwaombee ndogu zetu akina Roma, Monii, Bin Laden na mfanyakazi wetu Imma wawe salama maana hatujui wako wapi, mali si tatizo tatizo ni watu wangu kwanza mali zinanunuliwa lakini huwezi kununua roho ya mtu,” amesisitiza J Murder.

IMEANDIKWA NA
CHRIS BEE
+255718000262

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents