Michezo

Mnigeria kuzichapa na Klitschko

 

Bingwa wa uzito wa juu duniani Vladimir Klitschko anatarajiwa kutetea taji lake dhidi ya Samuel Peter wa Nigeria mnamo September 11 mwaka huu kwenye ukumbi wa Commerzbank-Arena jijini Frankfurt nchini Ujerumani.

Kambi ya Klitschko ilitangaza juu ya mpambano huo Ijumaa iliyopita ambapo bingwa huyo anayeshikilia mikanda ya IBF, WBO NA IBO atazipiga na Mnaija huyo akichukua nafasi ya Mrusi Alexander Povrtkin aliyekuwa ndiye mpinzani kwenye mpambano huo.

Povetkin, bingwa wa zamani wa Olimpiki alishindwa kutokea kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia mpambano huo.

“Nilipigana na Peter mwaka 2005, na ni kati ya mabondia wenye upinzani mkali niliyewahi kupigana nao” alisema Klitschko wakati akizungumzia pambano lao la mwaka 2005 ambapo Klitschko alifanikiwa kumshinda Samuel Peter.

Klitschko ambaye ni Raia wa Ukraine, meshinda mapambano 54 kati ya 57 wakati Peter ameshinda 34 kati ya 37.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents