Mnyama amalizia na Ubingwa wa Ligi Kuu Wanawake, aungurumapo Simba mcheza nani ?  

Timu ya Wanawake ya Simba Queens imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20 baada ya kushusha Gharika ya magoli mbele ya vijana wa Baobab Queen’s kwa jumla ya 5 – 0.

@simbaqueensctanzania imeshusha Gharika hiyo ya kipigo kwa Baobab Queen’s na kufuata nyayo za kaka zao @simbasctanzania kwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu kwa upande wa wanaume.

#simbasc walianza na Ubingwa wa Ngao Ya Hisani, Ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom msimu wa 2019/20, Ubingwa wa Azam Sports ASFC 2019/20 na sasa wameamuau kumalizia na Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2019/20.

Hakika kwa mafanikio hayo ni dhahiri shahiri Mnyama msimu huu alikuwa amejipanga hasa na wanastahili pongezi.

WRITTEN BY @fumo255
#Bongo5Updates #vodacompremierleague

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW