Burudani ya Michezo Live

Mnyama Simba alichukua na kombe la Azam Sports ASFC, aandika rekodi hii

Mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Mnyama Simba amefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports ASFC 2019/20.

Simba sasa inaandika historia kwa kuwa timu ya kwanza kuchukua kombe hili la Azam Sports ASFC zaidi ya mara moja.

Mnyama ameunguruma katika nyasi za Nelson Mandela Stadium kupitia kwa wachezaji wake Luis Jose Miquissone dakika ya 27’ na Nahodha John Bocco dakika ya 39’ ya mchezo.

Namungo wamejaribu kuchezea ndevu za Mnyama dakika ya 57′ kupitia kwa Edward Charles lakini hata hivyo walishindwa kufua dafu mbele Simba na mpira kumalizika kwa goli 2 – 1.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW