Michezo

Mnyama ‘Simba FC’ avutwa mkia Mwanza

Klabu ya Simba FC imelazimishwa sare ya goli 2-2 na klabu ya Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara mzunguuko wa nne.

Magoli ya Simba yamefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 16′ na Kotei dakika 49′ huku magoli ya Mbao FC yakifungwa na Habib Kayombo 47′ na Boniface Maganga 81′ yote yakifungwa kipindi cha pili.

Mchezo huo ambao umechezwa kwenye dimba la CCM Kirumba ulikuwa wenye upinzani wa hali ya juu baada ya Mbao FC kubadili mfumo wa ushambuliaji na kufanikiwa kupata magoli mawili.

Kwa sasa Simba wamebakia nafasi ile ile ya pili wakiwa na pointi 8 kwenye msimamo wa VPL huku klabu ya Mtibwa Sugar ikiongoza ligi kwa alama 9.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents