Michezo

Mnyama ‘Simba SC’ achinjwa Taifa na Bandari FC, matumaini ya Watanzania yabakia kwa Mbao FC

Klabu ya Simba imetolewa kwenye michuano ya SportPesa Super Cup kwa kukubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Bandari FC kutoka Kenya.

Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Kagere kunako kipindi cha kwanza na magoli yote ya Bandari FC yamefungwa kipindi cha pili.

Matumaini ya Watanzania kwa sasa yamebakia kwa Mbao FC pekee, kwani tayari Klabu ya Simba, Singida United na Yanga zimeshatupwa nje ya michuano hiyo ambayo mshindi atacheza na Everton ya Uingereza.

Bandari FC kwa sasa imetinga fainali na itasubiri mshindi wa mechi ya baadae kati ya Kariobangi Sharks na Mbao FC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents