Tupo Nawe

Mnyama Simba SC atwaa ubingwa TPL, Kagere na John Bocco wapeleka kilio Singida United

Klabu ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC imefanikiwa kunyakua kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 baada ya kuichapa Singida United goli 2-0 ugenini kwenye uwanja wa Namfua, Singida.

Simba wamefanikiwa kutetea ubingwa wao kupitia magoli ya Meddie Kagere dakika ya 10 na John Bocco dakika ya 60.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha alama 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi msimu huu. Huku Simba wakiwa bado wana michezo miwili mkononi.

Huu ni ubingwa wa pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita 2017/18 ikiwa njiani kuelekea Singida, na ni ubingwa wake wa 19 kwenye ligi hiyo, nyuma ya mabingwa wa kihistoria, Yanga ambao wameshachukua ubingwa huo mara 26.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW