Mnyika atembea Mabibo Makutano

John_Mnyika

Mbunge wa jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya Chama Cha CHADEMA Mh John Mnyika, juzi alifanya ziara ya kutembelea maeneo ya Mabibo Makutanao na kufungua tawi dogo eneo hilo. Katika Safari yake hiyo ambayo alikuwa akitembelea maeneo mbalimbali, aliweza kufafanua mambo mbalimbali ambayo wakazi wa eneo hilo yamekuwa yakiwatatiza kila kukicha.

Miongoni mwa majambo ambayo aliyafafanua, ni kuhusu barabara kutoka Mburahati ambayo  inakutana na barabara ya  chuo cha NIT, kwamba ipo katika orodha ya barabara zitakazo jengwa mwaka 2011 kwenda 2012.

Pia aliongeza kwa kusema barabara ya Ubungo External mpaka Ubungo Maziwa, ambazo amefanikiwa kwa namana moja ama nyingine kuongea na Tan Road na kuiweka katika mikakati ya ujenzi wa barabara hiyo.

John_Mnyik

Mheshimiwa Mnyika aligusia na tatizo la maji ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakazi wa eneo hilo, ila alisema matatizo ya maji yanapatiwa uvumbuzi baada ya kugundua sababu  zinazofanya maeneo hayo yawe na tabu ya maji.

Aidha alidai tatizo la kwanza ni utumiaji wa mota zenye nguvu kubwa kwa watu wachache kuvuta maji hata ya majilani zao, pili uhaba wa miundo mbinu ya maji ya eneo hilo.

Alisema pia matatizo ya vivuko vidogo vya watembea kwa miguu, wa maeneo hayo vimo katika majeti ya mfuko wa Mbunge, hivyo amewaomba viongozi wa mtaa kuweza kuwa macho na kuleta hoja katika kikao cha kamati ilikuweza kuzipitisha na kuzitendea kazi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents