Michezo

Mo ampa somo Emmanuel Okwi

Kiungo wa timu ya taifa ya Misri na klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza, Mohamed Salah alifanikiwa kuipatia timu yake ya taifa bao la ushindi wakati wakicheza dhidi ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia inayo tarajiwa kufanyika Urusi hapo mwakani.

Mo ameifungia timu yake ya taifa ya Misri dakika ya 6 katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano hiyo uliopigwa Alexandria nchini Misri na kulipa kisasi cha kipigo ilichopata nchini Uganda wiki iliyopita cha bao 1-0 kutoka kwa mchezaji wao anayekipiga katika klabu ya Simba, Emmanuel Arnold Okwi.

Shangwe zilitawala kwa mashabiki wa soka wa Misri baada ya kumalizika kwa mchezo huo, hii ni baada ya kukosa kushiriki katika michuano hiyo mikubwa tangu mwaka 1990 licha ya kushinda mataji manne ya Kombe la mataifa bingwa Afrika.

Matokeo hayo yanaifanya Uganda kubaki na alama 7 katika nafasi ya pili ya kundi E, na sasa itahitaji ushindi katika michezo yake miwili dhidi ya Ghana na Congo itakayopigwa Oktoba 6 na 8 mwaka huu huku ikiiombea dua mbaya Misri.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo iliyopigwa jana, Ghana imeishushia kipigo cha mabao 5-1 na kufikisha alama 5 katika nafasi ya 3 na kuiacha Congo ikibaki mkiani kwa alama 1.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents