Aisee DSTV!

Mo Dewji aandika ujumbe mzito adai hawezi kufanya kazi na mtu anayetoboa mtumbwi wanaosafiria

Katika siku mbili hizi kumekuwa na tetesi kuwa Mkurugenzi wa Bodi ya wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji huwenda akangatuka kwenye timu hiyo kutokana na kile kinachoelezwa kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya viongozi.

Image result for Dewji na Simba

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Mo Dewji ameandika kuwa ”Kwenye uongozi, na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa.”

”Kwenye uongozi, na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na sikubali kufanya kazi na mtu anayehujumu malengo, mipango na maslahi mapana ya taasisi – mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri nao.” – Dewji

Toka kuibuka kwa tetesi hizo, Mo Dewji amekuwa akiandika ujumbe mbalimbali na wenye mafumbo bila kukanusha ama kuweka wazi ukweli juu ya jambo hilo.

Hapo jana siku ya Alhamisi, Mkurugenzi huyo wa Bodi ya wadhamini ameandika ujumbe kuwa ”Watu wenye nia mbaya: Kazi yao sio kujenga, ni kuvunja tu. Kaa nao mbali. Narudia kaa nao mbali sana!.”

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW