Michezo

Mo Dewji atoa neno kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON kati ya Taifa Stars vs Lesotho

Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mo Dewji ametoa salamu za kheri kwa Timu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars katika kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho.

Image result for Mo Dewji simba
Mo Dewji

Dewji amesema kuwa ushindi wa leo dhidi ya Lesotho utaleta furaha kubwa kwa Watanzania, kwani ni miaka 38 tangu timu ya taifa ifuzu michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Nawatakiwa kila la kheri Taifa Stars katika mchezo wa leo dhidi ya Lesotho. Ushindi wa leo utarudisha furaha ya Watanzania ya kukosa kushiriki AFCON kwa miaka 38. Tunaamini mtafanya vizuri sababu nia tunayo na uwezo tunao. Mungu awe nanyi,“ameeleza Mo Dewji kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Taifa Stars ipo katika kundi L na inashika nafasi ya pili kwa alama 5, nyuma ya kinara Uganda yenye alama 13 baada ya kushinda  mchezo wa jana na kujikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo. Nafasi ya tatu ikishikiliwa na Cape Verde yenye alama 4 na Lesotho ikiburuza mkia kwa alama 2.

Stars itahitaji kushinda mchezo wa leo ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu AFCON 2019, ambapo itafikisha jumla ya alama 8 ambazo hata ikipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Uganda haitoweza kufikiwa na Cape Verde yenye  alama 4 endapo itashinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents