Afya

MO Dewji aungana na Waziri Makamba kuokoa maisha ya mwanafunzi wa KCMC anayehitaji Mil. 30 kupandikizwa figo

Mfanyabiashara Mohammed Dewji na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba wameonyesha kuguswa na tatizo linalomkabili mwanafunzi wa Chuo cha Tiba Kilimanjaro (KCMC), Arnold Augustine na kuhamasisha watu mitandaoni kumchangia mwanafunzi huyo fedha za matibabu.

Image result for januari makamba
Januari Makamba

Arnold (25) ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tano anachukua kozi ya udaktari KCMC anahitaji msaada wa Tsh milioni 30 kwa ajili ya matibabu ya kupandikizwa figo.

Awali Waziri Makamba ndiye aliyeanza kuendesha kampeni ya kupatikana kwa kiwango hicho cha fedha mitandaoni kwa kuanza kutoka milioni 6 na kuwahamamisha watu wengine kumuunga mkono.

Nimeongea na daktari na marafiki wa huyu yatima. Msaada unahitajika. Watu wengi wanahitaji msaada lakini tunaweza kuonyesha uwezo wetu wa huruma kwa huyu daktari. Sh10 milioni kabla jua halijazama. Naanza na Sh6 milioni from me na Salim Assas. Pledge mchango wako hapa.” ameandika Waziri Makamba kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Baadae MO Dewji naye akaahidi kutoa milioni 5 kupitia Taasisi yake ya MO Foundation kwa masharti kuwa endapo wadau wa mtandaoni watachangia milioni 15 yeye atamalizia kiasi kilichobakia.

Tayari watu mbalimbali mitandaoni wanaendelea kuchangia ili kufikisha milioni 30 ambapo kwa upande wa Wasanii wa muziki, Rapa Mwana FA naye ameahidi kutoa tsh milioni 2 milioni. Na wewe unaweza kuchangia chochote kwa kufuata maelezo haya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents