Michezo

Mo Dewji avunja ukimya kutimuliwa kwa Aussems, awaonya baadhi ya wachezaji ”Baadhi yao, huutumia kama fimbo ya kutuchapia”

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ameonyesha kutoridhishwa na nidhamu za baadhi ya wachezaji na kuongeza kuwa bodi ilichukua maamuzi magumu kwa kocha kutokana na sababu kama hizo. Timu imeshindwa kufikia malengo, kisha nidhamu hakuna na hivyo wakashindwa kuvumilia.

Image result for Mo Dewji vs aussems

Mo ameyasema hayo kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba ulofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Nyerere

“Siridhishwi hata tone na nidhamu ya baadhi ya wachezaji wetu nje ya uwanja. Nimekuwa mnyonge kuona uwekezaji tuliouweka kwao, baadhi yao, huutumia kama fimbo ya kutuchapia. Niwaambie wachezaji wote, Simba ni klabu kubwa kweli kweli, tena kubwa hasa, na hakuna shaka ni namba moja Afrika Mashariki, bodi ninayoiongoza mimi haitavumilia mchezaji yoyote asiyejua thamani ya Simba. Kuonyana onyana sasa imetosha.”- amesema Mo Dewji.

Mohammed Dewji ameongeza kuwa “Sisi tunawalipa vizuri mno, na wao wana wajibu wa kutulipa matokeo na furaha. Na ili furaha iwepo, lazima nidhamu isimamiwe kikamilifu, na katika hili hatutanii. Hatutajali ukubwa wa jina la mchezaji yoyote. Nidhamu kwetu ni muhimu kama tunataka tufikie malengo tuliyokusudia. Na haya ndio yaliyotufanya bodi tuchukue maamuzi magumu kwa kocha wetu. Timu imeshindwa kufikia malengo, kisha nidhamu hakuna, alafu tuvumilie ?”

Image result for Mo Dewji vs aussems

“Simba lazima tuamue kuteseka na moja katika mambo haya mawili, (1) tuzoee uchungu na maumivu ya nidhamu au (2) maumivu ya matokeo mabaya. Kama mpenzi wa Simba, siwezi, ”

“Mtaniwia radhi kidogo nimekuwa mkali ila nidhamu kwangu ndio kila kitu. Hata mimi mwenyewe naishi kwa nidhamu, na ndio siri ya mafanikio yangu, na naamini watu wote waliofanikiwa, na taasisi zote zilizofanikiwa msingi wake mkuu ni nidhamu ya kazi.”

“Klabu yetu imeimarisha sana timu zake za vijana na wanawake, na sasa sisi ni miongoni mwa klabu chache Tanzania zenye timu imara za vijana chini ya miaka 20, na ile ya miaka 17, na tuna timu nzuri ya wanawake, na tunazidi kuziimarisha.”

“Na katika msimu huu wa ligi, tutahakikisha tunachukua tena ubingwa ili tuje kuweka rekodi nyingine kwenye klabu bigwa Afrika. Nawahakikishia wanachama wenzangu kujikwaa si kuanguka, hatutarudia makosa! Insha’Allah, Mungu atutangulie.”- Mo Dewji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents