DStv Inogilee!

Mo Dewji awatumia ujumbe Simba kabla ya kuivaa Mbabane Swallows ‘Tunapaswa kuwa makini’

Mfanyabiashara maarufu nchini na muwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ameitakia ushindi timu hiyo ambayo inakabiliwa na mchezo wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Mbabane Swallows utakao pigwa hii leo majira ya saa 10:00 jioni.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter na Instagram, Mo Dewji ameandika ujumbe huo wa kuitakia mafanikio miamba hiyo ya soka nchini.

Nawatakia Simba kila la kheri katika mechi ya leo. Tunapaswa kuwa makini ili tufanye vizuri. Mungu awe nanyi na awazidishie nguvu na maarifa

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wataingia uwanjani kuwakabili Mbabane Swallows baada ya kupita miaka kadhaa pasipo kushiriki michuano hiyo.

https://www.instagram.com/moodewji/

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW