Michezo

‘Mo Ibrahim’ wa Simba awatumia salamu za vitisho Azam FC

Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Mohammed Ibrahim ‘Mo Ibrahim’ ametuma salamu za vitisho kwa klabu ya Azam FC kwa kusema kuwa kwa sasa klabu yake ipo tayari kuivaa Azam FC na kulipiza kisasi cha msimu uliopita.

Mohammed Ibrahim

Ibrahim amesema kwa sasa kikosi cha Simba kina njaa ya mafanikio na itakuwa vigumu kuziacha pointi tatu watakapokutana na Azam.

Simba na Azam zitakutana katika mchezo wa Ligi Kuu Jumamosi hii kwenye Uwanja Azam Complex, Chamazi, huku Simba ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa kwenye mchezo wa mwisho uliozikutanisha timu hizo.

“Tuna timu nzuri iliyokamilika, kukosa mabao ni sehemu ya mpira. Tunakwenda kujirekebisha kabla ya kucheza na Azam,”amesema Mo .

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema Simba itafanya vizuri kwenye mchezo wa Azam FC kwakuwa baadhi ya wachezaji wake muhimu watakuwa wamerudi kikosini.

Wanasimba wawe watulivu, kila mchezaji aliyesajiliwa ana nafasi yake. Niyonzima, Okwi na Juuko tumewakosa leo, lakini ni wachezaji muhimu. Kujiandaa kwetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo,”amesema Mayanja kwenye mahojiano yake gazeti la Mwanaspoti.

Jumapili iliyopita, Simba ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Hardrock ya Pemba na licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 washambuluaji Laudit Mavugo na Juma Liuzio walikosa mabao mengi ya wazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents