Burudani

Mo Music asikitishwa na maneno ya Timbulo

By  | 

Msanii wa muziki kutoka mkoani Mwanza, Mo Music amesema msanii mwenzake Timbulo kusema amemsaidia lakini hakutaka kutangaza hakuwa sahihi, kwani kusaidiana ni kitu cha kawaida.

Mo Music amesema anamuheshimu Timbulo kama msanii mwenzake na amemkuta kwenye game, lakini kitendo cha kusema amemsaidia sana ni uongo na hata suala la kutangaza anambania, halina ukweli wowote na hajapendezwa nacho.

“Timbulo ni kaka kwangu lakini anakuwa anakosea anapozungumza hivyo, kiukweli amenikwaza, Timbulo ni kaka ambaye nimemkuta kwenye muziki, anavyosema mimi natangaza ananibania ananibania nini, kwa sababu yeye ana mashabiki wake na mimi nina mashabiki wangu, hakuna faida yoyote”, alisema Mo Music.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments