Michezo

Mo Salah ni ‘MUNGU’ – Del Piero akunwa na uwezo wa mshambuliaji huyo hatari wa Liverpool

Legend wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia, Alessandro Del Piero amempachika jina jipya la Mungu ‘God’ mshambuliaji hatari wa Liverpool, Mohammed Salah kutokana na kuzidi kuwa tishio ndani ya uwanja tangu ajiunge Anfield akitokea Roma mwaka 2017.

Del Piero: Mohamed Salah is a

Nyota huyo kutoka kwa Mafarao wa Misri ameshuhudiwa katika msimu wake wa kwanza ndani ya ‘the Reds’ akipachika kambani jumla ya mabao 44 kwenye michezo 52 aliyocheza.

Katika msimu uliyopita Mo Salah, alifunga jumla ya magoli 27 huku hivi sasa akifumania nyavu mara 18 kiasi kwamba Del Piero amemvulia kofia kijana huyo.

Alessandro Del Piero has branded Liverpool forward Salah 'a God' after improving his game

Akizungumza na mtandao wa JOE, Del Piero amesema kuwa Salah ni Mungu ‘God’, ”Salah tayari yeye ni Mungu ‘God’ na hii sio tu kwa Misri.”

”Nakumbuka wakati alipokuwa Roma, mara kadhaa amekuwa mbele ya goli lakini alishindwa kufunga. Na ghafla akiwa Liverpool ameonesha uwezo wake kukua na kufunga zaidi ya magoli 30 kwa msimu.”

Alessandro Del Piero ameongeza ”Unapokuwa kwenye ubora wa namna hii, unahitaji kuimarika, kukuwa na hiko ni kitu kizuri.”

Del Piero mwenye umri wa miaka 45, amefunga jumla ya magoli 290 kwenye michezo yake 705 aliyopata kuitumikia klabu ya Juventus na amepata nafasi ya kumshuhudia Salah wakati huo alipokuwa akicheza ligi ya Serie A ndani ya klabu ya Roma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents