Burudani

Mobetto awapa kashikashi waandishi, aingia Red Carpet na baunsa

Mobetto awapa kashikashi waandishi, aingia Red Carpet na baunsa

Mrembo Hamisa Mobetto ambaye alikuwa host wa Miss Tanzania 2018 aliingia Red Carpet akiwa na mabaunsa ili kujikinga na waandishi wa habari ambao walimkimbilia kwa wingi baada ya kuonekana anaingia ukumbini hapo. Hata hivyo hakuna mwandishi ambaye alipata fursa ya kuzungumza naye zaidi ya Clouds Media ambao walikuwa wadhamini wa show hiyo.

Mobetto alikimbia kuongea na waandishi wa habari kwa kuhofia kuulizwa maswali ambayo alihisi yatamtoa kwenye mood kwani yeye ndio host wa sherehe nzima ya kumtafuta Miss Tanzania.

Siku kadhaa nyuma mrembo huyo alikumbwa na tetesi za kutaka kumloga baba wa mtoto wake Diamond Platnumz kwa madai ya kutaka gari pamoja na nyumba.

Shuhudi Mobetto alivyowakataa waandishi wa habari:-

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents